Thursday, May 27, 2010

Ufunguzi wa blog

Habari ya leo ndugu zangu wapendwa,
Leo blog mpya imefunguliwa. Ni sehemu ambayo kina mama tunazungumzia afya zetu, hasa uzito wa mwili wetu. Blog hii itakua inazungumzia jinsi ya kupunguza uzito na kutonenepa tena kwa ajili ya afya njema. Kama blog inavyosema "weigh right", ina maana uwe na uzito ambao mwili wako unaweza kubeba kwa ajili ya kuepuka "lifestyle diseases". magonjwa kama ya kisukari, high blood pressure, na moyo yote hayo yanaletwa na unene uliozidi, ukiondoa ya kurithi.
Nia ya blog hii ni kujadili jinsi ya kula zhakula kinachohitajika kwa ajili ya kupunguza unene. Pia kufanya mazoezi ili kuuweka mwili katika hali nzuri.
Mimi sio mwandishi kwa hiyo mtaniwia radhi kwa maneno machache ila kadri tunavyoendelea kutakua na majadiliano na ushauri mzuri tu. "watch this space"

No comments:

Post a Comment