Thursday, June 9, 2011

KULA VIZURI LEO KWA AJILI YA BAADAE

Natumai wote hamjambo kwa siku ya leo. Nimekua kimya tena na kama kawaida yetu lazima kuna sababu! "Naandika research yangu", "kazi zimekua nyingi" n.k. Ni kweli kwamba muda unakua mdogo kwa sababu ya mambo mengi ninayofanya lakini kama nikitaka kutafuta muda wa kufanya kitu nitaupata. Na leo nimeamua kupata muda na kuandika kitu kifupi tu.

Leo nataka kuzungumzia kuhusu kujiandaa sasa hivi kwa ajili ya uzee. Watu wengi huwa tunajiandaa kipesa kwa ajili ya maisha ya baadae. Lakini wachache sana tunakua tunajiandaa kiafya kwa ajili ya maisha ya uzeeni. Tunajua wote kwamba magonjwa mengi yanakua kwa wazee, blood pressure, kisukari, mzunguko mbaya wa damu n.k. Kitu ambacho huwa tunasahau wote ni kwamba hayo magonjwa tumekua "tunayaandaa" tangu tuko vijana kwa chakula tunachokula na lifestyle tunayofuata. Chakula tunachokula kama sio kizuri kwa miili yetu kinakua kinasababisha hali ya ugonjwa ambayo itakuja kujitokeza huko mbeleni.

Kwa hiyo basi, tuangalieni vyakula tunavyokula, tuchemshe badala ya kukaanga. Tutumie mafuta mazuri (olive oil, canola oil n.k). Tule samaki kwa wingi na kupunguza 'red meat". Na pia tusisahau kufanya mazoezi. hayo ni baadhi tu ya mambo machache tunayoweza kufanya kusudi tuwe na afya nzuri.

Nawatakieni afya njema

Farida