Friday, July 22, 2011

Watoto

Siku hizi watoto wetu wana "access" na vyakula vingi ambavyo sisi zamani tulikua tunaona kama ni luxury. Yogurt, Juice, Ice cream, sweets, biscuits na vingine vingi tu. Na sisi wazazi tunaona tusiwakatili raha yao na kuwapa hivyo vitu. Je, tunaangalia kiasi ambacho watoto wanakula hivyo vitu? Ukiangalia zaidi watoto wa siku hizi hawachezi kama tulivyocheza zamani. Kwanza mitaa siku hizi ina watu wengi na sio salama kwa hiyo hutaki kumruhusu mwanao akacheze mtaani, naelewa. Pili kuna michezo ya ndani ambayo pia sisi hatukuwa nayo, playstation, xbox, internet games, zote hizo zinawafanya watoto wasiwe na activities nje, wanakua na sedentary life.

Child Obesity ni shida siku hizi, watoto ma-obese wanazidi duniani. Unakuta watoto wana uzito wa mtu mzima na sisi wazazi tunajivunia kuwa na mtoto mnene, inaonyesha ni jinsi gani tunamlisha mtoto. Tunasahau kwamba watoto pia wanapata matatizo ambayo watu wazima wanapata wakiwa na uzito usiohitajika. Kuna kisukari cha watoto, watoto kutaniwa na wenziwe kwa unene walionao na hii inawashushia self esteem, n.k

Kwa hiyo mama na baba, tuwaangalie watoto wetu inapokuja suala la chakula, tuwape chakula kinachofaa na sio "junk food" zilizopo siku hizi. Tutakuwa tunawapenda zaidi kwa kuwapa hivyo vyakula kuliko kuwapa vyakula visivyofaa. Tuwahamasishe wacheze michezo ambayo itawafanya wawe active. Waruke kamba, waendeshe baisikeli, wakimbie n.k. Tukipata muda tucheze nao nje, itawasaidia wao na sisi pia. Kuna michezo mingi ambayo wazazi wanaweza kucheza na watoto, badminton, kuruka kamba, soccer au hata kufanya mashindano ya kukimbia hapo nyumbani. Itawapa mazoezi wote na pia muda wa ku-bond na mtoto. Kwa wale wanaokaa sehemu yenye bahari au ziwa, mnaweza kucheza michezo ya beach. Its fun and healthy!

Stay healthy