Friday, April 29, 2011

Muda

Ni muda mrefu sasa tangu nimetuma post katika hii blog. Sijivunii na kitendo hiki. Kama watu wote tusemavyo "muda sina kabisa siku hizi", mara tunasema "nitaanza kesho", "nitakapomaliza project hii nitaanza", n.k n.k. Muda hatuupati kama hatujitahidi. Kila siku tunakua tuna kitu tunafanya, na itakua hivyo hivyo mpaka mwisho wa maisha yetu. Leo nilikua naongea na mama mmoja ambaye anataka kupunguza uzito. Kaenda kumuona dietician (kalipa hela nyingi tu) lakini hakuchukua karatasi aliyopewa kwa ajili ya kuanza program. Nilivyokua naongea nae sikuona kama ana nia ya kupunguza uzito, niliona anataka kufanya hivyo kwa sababu anajua inabidi afanye hivyo lakini hajui kama ataweza kufanya hii programm.

Sasa basi, watu wengi ambao wanataka kupunguza uzito wanakua na nia ya kupunguza uzito lakini hawana "nguvu" au imani kwamba uzito utapungua. Hii ni kwa sababu wamejaribu "njia nyingi" ikiwa ni pamoja na kujishindisha njaa ili kupunguza uzito. Kwa hiyo wanaamua kusema kwamba hawataweza. Mpaka kuwa na "turning point", labda ugonjwa au kitu kingine. Lakini utakuta mpaka muda huo ufike inakua ni vigumu zaidi kufuata afya nzuri.

Nakumbuka mume wangu kabla hajaanza program alitaka kununua saizi kubwa ya nguo sababu alizokua nazo zilikua zimeanza kumbana. Alishindwa kumbeba binti yetu vizuri sababu tumbo lilikua linamsubua na siku hiyo ndio tukaamua kwamba anaanza program!, hiyo ndio ilikua "turning point" yake. Manake tukaona sasa tutanunua nguo kubwa mpaka lini? Wiki iliyofuata akaanza kufuata "helathy lifestyle" rasmi. Na baada ya miezi minne alikua ameshafikia kwenye uzito unaofaa, na ni mwaka sasa yuko katika uzito huo huo.

Kwa hiyo ndugu zanguni tutafute "turning point" yetu wakati bado tunaweza kusudi tuweze kuanza kuangalia uzito wetu. "Turning point" yetu inabidi tuipate wakati bado tunaweza, sio kwa sababu tunaumwa sababu wakati huo unaweza kushindwa kufuata hii "lifestyle" kwa sababu ya ugonjwa.

"Turning point" zetu ziko nyingi kama tukizitafuta. Miguu kuuma, uzito wa mwili kwa ujumla, mama ana blood pressure kubwa, baba wa jirani kafariki ghafla kwa stroke, n.k, n.k. Hizi zote ni hali ambazo ukifuata "lifestyle" nzuri ya kula utaepuka matatizo haya.

Tuanze kuangalia afya zetu wakati bado tunaweza, huko mbele inakua vigumu zaidi na inakua "expensive" zaid sababu inaunganisha matibabu na kila kitu.

Nawatakieni afya njema