Wednesday, September 8, 2010

Uzito mzuri kwa afya nzuri

Kwa mama wa kiafrika mwenye mtoto wa watoto, unene ni kitu ambacho kinakubalika na kinachukuliwa kama ni maisha mazuri. Kila wakati utasikia mtu anasema "nimemuona fulani kanenepa kapendeza!" Unene umekua ukihusishwa na "mafanikio" ya maisha. Lakini siku hizi watu wengi wameona kwamba unene "sio dili" tena, ni mzuri kama bado uko kijana, active na nguvu zako. Japo unakua unaipa miguu uzito mkubwa wa kubeba mwili mnene, unakua hausikii sana sababu bado una nguvu zako. Sasa basi ikifika wakati miguu inachoka kubeba mwili mkubwa, moyo unakua umezungukwa na mafuta, mishipa inakua ina mafuta na mzunguko wa damu unakua wa shida, ndio hapo unaona tunaanza kuwatatata "maspecialist" kwa ajili ya magonjwa mbalimbali, hypertension, high cholestrol, kisukari, magonjwa ya moyo to name few.
Sasa ndugu zangu, ni wakati ambao inabidi tuangalie miili yetu kwa ajili ya watoto wetu, waume zetu na hasa hasa kwa ajili yetu wenyewe. Wakati ule wa kusema "unene dili" umepita na tujiangalie miili yetu, weather tuna watoto au hatuna, uzito wetu tunaweza kuungalia na kuuweka katika "uzito mzuri", kama blog hii inavyosema.
Nawatakia afya njema