Friday, April 20, 2012

Penye Nia

Habari ya leo ndugu zangu katika afya njema. Leo nimerudi tena baada ya kimya kirefu (msinichoke!). Leo nataka kuzungumzia kuhusu mdogo wangu Rukia Goronga. Kwa kweli nimefurahishwa na amenifanya nijivunie kwa nia yake ya kupoteza uzito. Aliamua kuufanyia kazi uzito wake na kweli amefanikiwa. Alikua ana uzito wa kutishia afya yake, uzito wa 93kg sio uzito wa kuwa na mtu anayetaka afya njema. Lakini leo najivunia kusema mdogo wangu ameweza kupunguza kilo zaidi ya 20!Ndio, umesoma vizui, kg 20! kwa sasa ana 71.6kg kwa kweli anahitaji pongezi nyingi. Sasa hivi anajisika ana nguvu zaidi, kazini anaenda kwa kishindo chote, amebadilisha nguo zote sababu hakuweza kuvaa nguo za zamani tena. Ni hela ambayo anafurahi kuitumia kwa kununua nguo saizi ndogo kwa sababu anapendeza zaidi ya nguo zake za zamani. Way to go lil sis!

Hii inaonyesha kwamba tukitaka kitu kwa moyo wetu wote tutafanya tu, na tukiwa na watu ambao wanatusaidia kimawazo basi tutafika tunapotaka.

Nawaomba ndugu zangu, mkitaka kufanya kitu mnaweza ni kujiwekea malemgo na sababu ya kufany hicho kitu! Wengine wanaamua kuacha kunywa pombe sababu ya watoto, wengine sababu ya dini, wengine sababu ya kazi na wengine sababu ya afya zao. Sasa wewe unaamua kupunguza uzito kwa sababu gani? Sababu kubwa na ya umuhimu ni kwa ajili ya afya yako! Itunze hiyo afya yako, utunze huo mwili wako manake unao mmoja tu! I am challenging you to take action and take care of your health, you will love yourself more after this!

Wenu katika afya!
Farida

No comments:

Post a Comment